top of page

キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira - Habari kutoka Kingolwira -No.10

Hali ya hewa kwa mwisho wa mwaka huu ilikuwa ni hali ya jua kali (ukame) hakukuwa na mvua kama kawaida ya miaka mingine ambayo mvua hunyesha kiasi kwa ajiri ya kustawisha matunda kama embe, machungwa na kiasi mananasi. Kwa hiyo wakulima wanatarajia kuvuna matunda toka shambani kiasi kidogo kutokana na ukosefu wa mvua ya kutosha.

Pia ni kawaida mwezi wa mwisho wa mwaka (December) wakulima huanza kutayarisha mashamba yao tayari kwa kupanda mazao mbali mbali lakini mwaka huu kasi ya kutayarisha inakwenda taratibu sana kutokana na hali ya ukame.

Mwaka huu 2010 katika kijiji cha Kingolwira wanakijiji walikuwa na shughuli ya UCHAGUZI. Uchaguzi huu ulikuwa wa viongozi wa kijiji yaani serikali za mitaa na baadaye mwezi wa kumi ukafanyika uchaguzi wa viongozi wa juu Mbunge na Raisi.

Kijiji cha Kingolwira hutembelewa na wageni toka nje wakiwemo Wajapani kwa mwaka huu mwezi wa tisa wanafunzi toka chuo kikuu cha Ryukoku ya Kyoto, Japani walitembelea kijiji walipata nafasi ya kuzungumza na wanakijiji hasa vijana na kutembelea maeneo kama shambani na pia walipata nafasi ya kutembelea kijiji cha jirani cha Mkambalani.

(1/01/2011)


今年の年末は、マンゴー、オレンジやいくつかのパイナップルを実らせるための例年の雨と違って日差しが強く(旱魃)雨の少ない天候でした。ですので、農民たちは、雨不足のためにわずかの果物の収穫しか期待できません。

例年なら年末の12月には、農民たちは、様々な作物の植え付けの準備を始めているのですが、今年は、旱魃のためにその準備のスピードもとてもゆっくりしたものとなっています。

今年は、村人には選挙がありました。選挙は、村の代表を選び、そのあと10月に国会議員と大統領の選挙もしました。

9月には、日本からの龍谷大学の学生も迎えました。学生たちは村を歩き、村人たち、とくに若者たちと話をしました。畑などへも行き、近隣の村、マカンバラーニ村へ行く機会もありました。

(2011年1月1日)

グビさんの畑。9月撮影/Shamba la Ngubi,Mwezi wa 9
村の子どもたち/Watoto wa kijijini

閲覧数:4回0件のコメント

最新記事

すべて表示

JATAツアーズのスタッフたちが綴るタンザニアをご紹介します。 ​【目次】 ​ ★Kusikia si kuona(百聞は一見にしかず) - 相澤 俊昭 ★Tunatembea - 白川 千尋 ​ ★Habari kutoka Lukani(ルカニ村ニュース) - アレックス(ルカニ村出身) ​ ★Habari kutoka Kingolwira(キンゴルウィラ村ニュース) - グビ、ハミシ、ヤウ

記事: Blog2_Post
bottom of page