top of page
  • 執筆者の写真白川

キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira - Habari kutoka Kingolwira -No.11

サルム・グビ Salum NGUBI

Katika msimu wa mwanzoni mwa mwaka 2011 kijiji cha Kingolwira kilipata hali ya hewa ya ukame kiasi cha kutia wasiwasi kwa wakulima. Lakini kwa bahati nzuri hali ya hewa ilibadilika ghafla mnamo mwezi wa pili yaani February mwanzoni mvua ilianza kunyesha na kuendelea. Wakulima walizitumia mvua hizo kwa kupanda mazao ya aina mbalimbali kama vile mahindi,mpunga,viazi vitam muhogo na kadhalika.

Mvua ziliendela mpaka katikati ya mwezi wa sita na iliwapa wakulima tija; Waliweza kuvuna mazao ya matunda mengi kama vile machungwa,ndizi,mapera,na hata miwa. Mwaka huu ni mzuri kwa Kijiji cha Kingolwira na Mkoa wa Morogoro kwa ujumla. Pia mwaka huu ni mzuri kwa Wakulima kwa kuwa wanaweza kuuza mazao yao na kupata pesa ambazo zitawawezesha kununua mahitaji ya kila siku.

Mbali na shughuli za kilimo Wanakijiji pia wanajiandaa kufyatua matofali ya udongo na baadaye watayachoma, kazi hii hufanywa hasa wakati wa kiangazi yaani baada ya mvua za masika kwisha ambazo hivi karibuni zimeisha. Kwa kawaida kazi hii hufanywa na vijana kwa sababu ni kazi inayohitaji nguvu kwa hiyo watu wenye umri mkubwa mara nyingi hushindwa kufyatua matofali, matofali hufyatuliwa na kuchomwa na yakiwa tayari Vijana husubiri wateja wa kununua. Watu hawa mara nyingi ni Wanakijiji.

Kwa kawaida Wanakijiji baada ya mavuno ya mazao yao toka shambani hujishughulisha na maandalizi ya sherehe za mila, hii ni pamoja kuandaa ngoma za kienyeji, maana kubwa ya sherehe za ngoma hizi ni kwa ajili ya kusherekea watoto kutimiza umri wa utu uzima,wakati huu kijana hasa wa kike atakua kati ya miaka 14 hadi 17 umri huu anapaswa kufanyiwa sherehe na nia hasa kupewa maadili ya kuwa mtu mzima.

Kwa kuwa Kijiji cha Kingolwira kipo kando kando ya barabara kuu iendayo mikoa ya kati na magharibi ya Tanzania na nchi jirani, kama vile ZAMBIA,RWANDA,BURUNDI,DRC na kadhalika, kwa hiyo imeonekana kuna tatizo kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kwa vijana, kwa hiyo kijiji kimetafuta wakufunzi wa kufundisha rika kuhusu ukuaji na rika ili waweze kujiepusha na ugonjwa wa ukimwi.

MWISHO,imetayarishwa na Ngubi

(15/07/2011)


 2011年の初めのキンゴルウィラ村は、農民を心配させるほどの乾燥した天候でした。が、幸運なことに、第二の月つまり2月初めに急に天候が変わり、雨が降 り始め、そのまま降り続きました。この雨で農民たちは、とうもろこし、稲、さつまいも、キャッサバなどさまざまな種類の作物を植えることができました。

 雨は6月半ばまで降り続き、それによって農民たちは生産性を高めることができ、オレンジ、バナナ、グアバやサトウキビまで、たくさんの果物が穫れました。 全体的にキンゴルウィラ村、そしてモロゴロ州にとっては、今年はよい年になりました。 農民たちにとっても、作物を売り、日々の必要を満たすお金を得ることができるので、やっぱりよい年です。

 農業の他にも、農民たちは土のレンガを作り、後に焼く準備をします。この仕事は、つい最近終わった雨季の後の、乾季によく行われます。通常この仕 事は、若者が行います。というのも、レンガ作りはとても力の要る仕事で、年配者にはレンガ作りはきつい仕事です。レンガを作り焼いて出来上がると、若者 たちは買いに来るお客さんを待ちます。これらの人々の多くは村人です。

たいてい畑の作物の収穫が終わった後は、村人たちは伝統のお祝いの準備に取りかかります。このお祝いには地元の太鼓も用意されます。太鼓を用いた祝宴の目 的は、成人の段階に入る年齢に達した子どもたちをお祝いすることにあります。このとき14歳から17歳の女の子たちは、祝われ、成人になるための道徳を教えられます。

キンゴルウィラ村は、タンザニアの中央部や西部の州、また隣国のザンビア、ルワンダ、ブルンジ、コンゴ民主共和国などに続く幹線道路沿いにあるので、若者たち のエイズの感染という大きな問題が見られます。村は若者がエイズを予防することができるように、彼らに若者同士の関係について教えることのできる人材を探 しています。

(2011年7月15日)

サイザルの畑を行く/Shamba la Mkonge
料理/Upishi

閲覧数:4回0件のコメント

最新記事

すべて表示

JATAツアーズのスタッフたちが綴るタンザニアをご紹介します。 ​【目次】 ​ ★Kusikia si kuona(百聞は一見にしかず) - 相澤 俊昭 ★Tunatembea - 白川 千尋 ​ ★Habari kutoka Lukani(ルカニ村ニュース) - アレックス(ルカニ村出身) ​ ★Habari kutoka Kingolwira(キンゴルウィラ村ニュース) - グビ、ハミシ、ヤウ

記事: Blog2_Post
bottom of page