top of page

キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira - Habari kutoka Kingolwira -No.14

サルム・グビ Salum NGUBI

Katika mwaka huu wa 2012 mwanzoni hali ya hewa ilikuwa ya wastani mvua ilikuwa kiasi, si ya kutosha kufanya mazao mengi kustawi vizuri wakulima wengi walivuna mazao kiasi kidogo kulinganisha na mwaka uliopita wa 2012.

Kutokana na hali ya hewa mbaya, wanakijiji wameshauriwa kupanda mazao yanayo stamili ukame ili kuepuka kukosa chakula cha kutosha,mazao hayo ni kama vile mtama-millet, muhogo kunde kwa mazao ya chakula mazao biashara ni ufuta,alizeti ushauri ulifanywa na Wataam Kilimo kutoka makao makuu ya mkoa Morogoro, Wakulima na Wataalam kwa pamoja walikubaliana msimu huu yaani mwishoni mwa 2012 na mwazo wa 2013 kufanya shamba Darasa yaani shamba la mfano litakalo kuonyesha Kilimo cha kisasa [Kilimo bora],Na Wataalam waliwapa mafunzo Wakulima wenye mashamba karibu namna yakumwagilia mazao [irrigation system] wakati wa uhaba wa mvua.

Mbali na kupata mafunzo ya kilimo, wanakijiji pia walifanya maandalizi ya sherehe zao ambazo hufanyika kila mwishoni mwa mwaka, kama kawaida sherehe hizi zinahusika sana na wasichana ambao wamekua na umri kati ya miaka kumi na tano na kabla ya miaka kumi na nane. Sherehe za kumuelimisha kijana, msichana kuwa sasa anaingia katika umri wa utu uzima kawaida sherehe hufanyika kwa kucheza ngoma za kienyeji lakini siku hizi baadhi ya watu wanalaumiwa sana kwani badala ya kupiga na kucheza ngoma za kienyeji wanacheza muziki hasa rusharoho.

Mwanzoni mwa 2012 Wanakijiji wa Kingolwira walipokea wageni toka Japan ni wanafunzi wa Chuo kikuu cha MEIJI GAKUIN ni Wanafunzi wanane ambao Waliongozana na Prof. wao Katsumata. Wanafunzi hao walitembelea sehemu mbalimbali kama vile shule ya msingi, sekondari pia walitembelea shamba na Walioongea na baadhi ya Wanakijiji, wote kwa pamoja walifurahi. Baadae kilifuata vikundi viwili cha kwanza watu wanne kilichoozwa na Mr.Shimogaki na kingine ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ryukoku kikiwa na Wanafunzi kumi na nane wote. Kama wageni waliopita nao walifanya kama hivyo na wote kwa pamoja walifurahi kutembea Kijiji cha KINGOLWIRA na Wanakijiji pia walifurahi has hasa vijana.

(01/11/2012)


今年2012年の初めは、多くの農作物にとって雨量が十分ではなく、多くの農民たちが昨年と比べて少ない農作物を収穫することとなりました。

悪天候の影響を受け、村人たちは、食糧が不足しないように日照り続きにも耐えうる農作物を植えるよう、専門家との話し合いで助言を受けました。それら農作物とは、村での消費用のモロコシ、キャッサバ、ササゲ豆、そして換金用のゴマとヒマワリです。この話し合いは、モロゴロ州本部から派遣された農業専門家と共におこなわれました。話し合いの中で、農民たちと専門家は、今季、つまり2012年末から2013年初めにかけて畑公開をおこなうことに合意しました。つまり、ある畑で最新のよりよい農業を実践し公開するのです。そして、近くに畑を持つ農民たちは、専門家から雨不足の際におこなう灌漑の方法を教わりました。

専門家が来て農業について学んだ出来事以外に、村人たちは、毎年年末におこなわれるお祝いの準備もおこないました。大抵この祭りは、15歳から18歳になる前の女の子に大きく関係するもので、教育を受け成人になろうとしている若者、特に女の子を祝うためのものです。このお祝いではいつも村の太鼓をたたき踊って祝うのですが、最近ではそれに不満を言う人が幾人かでてきました。なぜなら彼ら若者は、村の太鼓をたたいて踊るよりも、音楽をかけて踊ったり歌ったりする方を好むからです。

2012年の初め、キンゴルウィラの村人たちは日本からのお客さんを迎えました。明治学院大学の勝俣教授率いる8名の学生たちです。学生たちは、小学校や中学校、畑など様々な場所を訪問して村人たちと話をし、学生も村人も楽しく過ごしました。その後続いて2つのグループが村を訪れました。1つ目のグループは下垣さん率いる3名(AT:オルタナティブツアー)、2つ目のグループは龍谷大学の18名の学生たちです。彼らも同様に過ごし、キンゴルウィラ村を一緒に歩いて楽しみました。村人たちも、特に若者はとても喜んでいました。

(2012年11月1日)

ATで来た青年と子どもたち/Kijana Mjapani na watoto wa kijijini©関口慶太郎
市場でお買い物/Ananunua mboga sokoni©横田彩子

閲覧数:4回0件のコメント

最新記事

すべて表示

JATAツアーズのスタッフたちが綴るタンザニアをご紹介します。 ​【目次】 ​ ★Kusikia si kuona(百聞は一見にしかず) - 相澤 俊昭 ★Tunatembea - 白川 千尋 ​ ★Habari kutoka Lukani(ルカニ村ニュース) - アレックス(ルカニ村出身) ​ ★Habari kutoka Kingolwira(キンゴルウィラ村ニュース) - グビ、ハミシ、ヤウ

記事: Blog2_Post
bottom of page