キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira - Habari kutoka Kingolwira -No.18
Hamisi Abdallah
Kufika Kingolwira
Kufika Kingolwira kutoka Dar tunatumia usafiri wa mabasi. Tunapendelea zaidi kutumia Abood Bus kwa safari salama na uhakika. Kijiji kipo umbali wa kilometa kumi kutoka mjini, kando kando ya barabara kuu ya kwenda mikoani. Bodaboda, baiskeli na daladala hutumika kwa usafiri wa ndani na nje ya kijiji.
Mazingira
Kingolwira imezunguukwa na milima ya Uluguru pande zote ambayo ndio chanzo kuu cha maji. Mashamba makubwa ya mkonge yamechukua sehemu ya ardhi yake yenye rutuba. Mto Ngerenge na Kitungwa imepita kwa upande wa kaskazini na magharibi ya kijiji. Uwepo wa mito hiyo unatoa fursa kwakilimo cha umwagiliaji na shughuli za utengezaji matofari.
Wenyeji
Wenyeji wa Kingolwira kwa kiasi kikubwa ni Waruguru, pia wapo Wakwele, Wakami, Wazigua,Wakaguru na Wamasai. Kutokana kupitwa na barabara kuu ,kwa sasa kuna mwingiliano mkubwa na makabila ya bara zaidi kama Wasukuma, Waha,Wanyamwezi n.k. Mwingiliano huu umeleta changamoto kiuchumi na kiutamaduni kwa wenyeji.
Shughuli za Maendeleo
Kilimo ndio shughuli kuu kwa wenyeji kwa kiasi kikubwa, pia vijana wanachangamkia fursa nyingine zinazojitokeza. Uanzishwaji wa nyumba za kulala wageni, maduka, mabaa na migahawa ya vyakula imepamba moto kwa sasa. Ongezeko la watu linaongenza uhitaji wa bidhaa za viwanda na kilimo hivyo soko la mazao linakua pia.
Hali ya Sasa
Sasa ni kipindi cha vuli, wakulima wameaandaa na kupanda. Mvua zinanyesha kiasi cha kuridhisha. Miembe imealika maua na kutoa matumaini kwa wakulima. Shughuli za matofari pia zinaendelea vizuri pia kwa kuwa mvua zinazonyesha si kubwa sana kutishia uzalishaji. Kwa ujumla maisha yanaendelea vizuri yenye matumaini kwa kila aneyejishughulisha .
AHSANTE.
(15/12/2014)
キンゴルウィラへ ダルエスサラームからキンゴルウィラへの交通はバスです。アブードという会社のバスが、安全で確実なので、よく使います。キンゴルウィラはモロゴロの町から10㎞で、幹線道路沿いです。村の中では、ボダボダ(バイクタクシー)や自転車、ダラダラ(乗合バス)などを移動手段で使います。
環境 キンゴルウィラは四方を、水源地でもあるウルグル山脈に取り囲まれています。広大なサイザル麻の農場が肥沃な土地を占めています。ンゲレンゲ川とキトゥンガ川が村の北と西に流れています。この川があるので灌漑とレンガ作りができます。
村人たち 村人のかなり多くはルグル人です。また。クウェレ、カミ、ジグア、カグル、マサイ人もいます。幹線道路が交差することによって、現在、いろいろな民族がやってくるようになりました。スクマ、ハ、ニャムウェジ人などなど。こうしたことは、村人たちに経済や文化への課題をもたらしています。
発展すること 農業は村人たちにとってもちろん主要な生業です。若者たちは、別の新しいことに挑戦しています。旅行客のためゲストハウスや、店、バーや食堂は今とてもホットな感じで増えています。増加した人口は工業製品や成長する農業市場も必要としています。
現在のこと 今は小雨季です。作物の植え付けの準備をしています。十分な量の雨が降ります。マンゴーの木は花をつけ、農民たちに希望を与えています。レンガ造りも順調ですが、雨量があまり多くないとよくない影響が出るでしょう。希望を持って仕事に取り組んでいる人びとにとって、全般的に生活はよくなっています。
読んでくださってありがとう。
(2014年12月15日)
にぎわう市場/Soko
サイザル麻とウルグル山/Mkonge na milima ya Uluguru
©Ayo Peter