top of page
  • 執筆者の写真白川

キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira Habari kutoka Kingolwira -No.25

Yaummy Nyombe


※日本語訳が下にあります。

Tangu kuanza kwa mwaka 2017 katika mkoa wa Morogoro kulikua na mvua nyingi sana kati ya mwezi wa march mpaka mwezi wa june mwishoni hivyo kuwawezesha wakazi wa kijiji cha Kingolwira kufanya kilimo cha mazao mbalimbali kwa wingi zaidi ikiwemo mahindi, Mpunga, Mtama, Nyanya maji, nyanya uchungu, matikiti maji,Matango nk. Na kufanikiwa kupata mazao mengi na yenye mafanikio kabisa kwa mwaka huu wa 2017/2018 , kwa mafanikio hayo kijiji cha Kingolwira hakitakua na njaa kabisa kwa mwaka huu.

Mnamo tarehe 22 Aug Kijiji cha Kingolwira tulifanikiwa kupata wageni wa Altenative Tour (AT) kutoka nchi rafiki na Tanzania yaani kutoka Japan. Katika safari hiyo tuliweza kutembelea sehemu mbalimbali jirani na kijiji cha kingolwira kikiwepo kijiji cha Kiegea ambacho ni umbali wa Kilomita Nane kutoka kijiji cha Kingolwira, huko tuliweza kwenda kuona maisha halisi ya kabila la wamasai na wakatukaribisha vizuri sana tukanywa na chai ya maziwa ya Kimasai. Baada ya kutoka kijiji cha wamasai tulipita katika shamba la bw. Hamisi Ngubi na kuona jinsi anavyoandaa shamba lake kwa ajili ya kilimo cha nyanya za umwagiliaji ambazo hulimwa wakati wa kiangazi yaani wakati wa jua kali, na hii hufanyika mara tu baada ya kumaliza kuvuna mahindi yaliyo kua yamekauka katika shamba hilo hilo. Pia kesho yake tulitembelea katika shule ya msingi Kingolwira na kuweza kuwapa msaada wa vitabu kidogo pia tukaona baadhi ya madarasa na ofisi ambavyo vilijengwa kwa msaada kutoka kwa watu wa Japan, mwl mkuu wa shule hiyo bw Jimmy alitukaribisha vizuri na kuweza kuwa na muda mzuri wa watoto wa darasa la sita ambalo tuliweza kuingia darasani kwao na kuongea nao vizuri.

Vilevile mwaka huu wa 2017 baadhi ya wafanyakaji wa Jata Tour waliweza kufanya safari ya kutoka Dar es salaam na kwenda katika kijiji cha kingolwira kwa ajili ya kwenda kuzuru katika kaburi la aliyekua mmoja wa wanzilishi wa kampuni ya Jata Tours aliyefariki mnamo mwaka wa 2013 Marehemu Salum Ngubi. Wafanyakazi hao wakiambatana na Bw. Hamisi pia walifanikiwa kupita katika eneo lingine hapo hapo kijijini na kwenda kuona kaburi alikozikwa mmoja wa madereva aliyewahi kufanya kazi Jata Tours marehemu Rahib Nyombe aliyefariki mwaka wa 2014. Pia mnamo tarehe 23 mwezi wa tisa aliyekuwa mfanyakazi wa Jata tours miaka nane aliyopita Bi Chiho IKEDA naye pia akiambatana na mume wake walifanikiwa kwenda kuzuru kaburi la merehemu Salum Ngubi yeye kwa sasa aniashi nchini japan

Kwa ufupi hizo ndizo habari za kutoka kijiji cha kingolwira kwa mwaka huu wa 2017

(15/11/2017)

2017年初頭からモロゴロ県の雨量は多かったです。雨のおかげで、3月から6月の終わりにかけて村人たちがトウモロコシ、コメ、モロコシ、トマト、ニャニャチュング(見た目はトマトだけどナスのような野菜;訳注)、スイカ、キュウリなどを含む多くの様々な作物を作りはじめることができました。 2017/2018年は豊作となり、今年は村人たちがお腹を空かす心配は全くないでしょう。

8月22日に村にはタンザニアの友だちの国、日本からオルタナティブツアー(AT)のお客さんを迎えることができました。いろいろなところへ行きました。キンゴルウィラ村の近くのキゲラ村も訪問しました。ここは、キンゴルウィラ村から8km離れていて、マサイの人々の生活に触れることができます。彼らはあたたかく迎えてくれ、マサイのミルク入りチャイを振舞ってくれました。

その後、ハミシ・グビさん(村のホスト;訳注)の畑に行き、太陽の光の強い乾季に栽培されている灌漑用のトマトをどのように準備しているのかを見ました。これは、この畑で乾いたトウモロコシを収穫した後に行われます。

翌日は、キンゴルウィラ村小学校を訪れました。子どもの本を少し寄贈し、日本の援助で作られた教室や事務室を見学しました。校長先生のジミーさんは、わたしたちをとても歓迎してくれました。6年生の教室に入り、子どもたちと話をする時間も十分ありました。

また、ジャタツアーズのスタッフたちもダルエスサラームから村にやってきました。2013年に他界したジャタツアーズの創業者の一人である故サルム・グビさんのお墓参りのためです。ハミシもまじえたジャタツアーズのスタッフたちは、2014年に他界したジャタツアーズでも仕事をしたことのある運転手故ラヒブ・ニョンベさんのやはりキンゴルウィラ村にあるお墓参りもしました。

9月23日には8年前にジャタツアーズの社員で今は日本に住んでいる池田智穂さんもおつれあいと一緒にキンゴルウィラ村にグビさんのお墓参りに来てくれました。

これが今年のキンゴルウィラ村からのお知らせです。

(2017年11月15日)

お墓へ向かう道/Njia ya kwenda makabirini
ヒマワリ油をとるためのヒマワリ畑/Shamba ya alizeti

閲覧数:21回0件のコメント

最新記事

すべて表示

JATAツアーズのスタッフたちが綴るタンザニアをご紹介します。 ​【目次】 ​ ★Kusikia si kuona(百聞は一見にしかず) - 相澤 俊昭 ★Tunatembea - 白川 千尋 ​ ★Habari kutoka Lukani(ルカニ村ニュース) - アレックス(ルカニ村出身) ​ ★Habari kutoka Kingolwira(キンゴルウィラ村ニュース) - グビ、ハミシ、ヤウ

記事: Blog2_Post
bottom of page