キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira - Habari kutoka Kingolwira -No.4
サルム・グビ Salum NGUBI
Kingolwira kwa sasa hali ya hewa ni joto na mvua nyingi kiasi, kwa kawaida mwezi wa April, May ni wa mvua (Masika) lakini mwaka huu hakuna mvua nyingi, pia kwa sasa na msimu wa matunda kama machungwa na mapapaya. Wanakijiji kwa sasa wanashughulika na shughuli za kilimo kama mahindi viazi vitamu na nyanya, lakini kuhusu mpunga hali ya hewa si nzuri kwa hiyo wakulima wamepata hasara, hawataweza kuvuna mpunga.
Wanakijiji pia wamefurahia kwa kufunguliwa kiwanda kipya cha matunda ambacho kipo karibu na kijiji kama kilomita 1.5. Kiwanda ambacho wanategemea kuuza matunda yao kutoka mashambani na hasa kwa sababu kiwanda ni kikubwa.
Pia wanakijiji wanatarajia kufunguliwa kwa kituo kipya cha afya (Health Centre). Ufunguzi wa sherehe unategemea kufanyika hivi karibuni. Kituo cha afya ambacho kitakuwa na uwezo wa kusaidia kama vijiji vitatu vya karibu.
(1/6/2007)
キンゴルウィラ村は今は暑く雨の多い季節を迎えています。例年4、5月はMasikaといわれる大雨季ですが、今年はそれほど多く降っていません。そして今はオレンジやパパイヤといった果物の季節でもあります。村人たちはとうもろこしやさつまいもやトマトなどの作物の農作業に取りかかります。でも、米作りにはこの気候はよくありません。農民は米の収穫ができないだろうから、がっかりしています。
村人たちは新しい果物の集荷場が村から1.5kmと近いところに開かれるので喜んでいます。この集荷場では畑から収穫した果物を売ることができます。とっても広い集荷場なのです。
また村人たちは新しい診療所が開くのを心待ちにしています。開所式はもうじき行われるでしょう。この診療所が開くと近隣の3つの村の人々が診察を受けることができるようになります。
(2007年6月1日)
新しい診療所の看板
診療所建設中!