top of page

キンゴルウィラ村便り/Habari kutoka Kingolwira-Habari kutoka Kingolwira -No.5

サルム・グビ Salum NGUBI

Katika kijiji cha Kingolwira hali ya hewa katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, ni mvua kiasi na hali ya joto hasa nyakati za mchana. Ni kipindi cha kuandaa kilimo ingawa baadhi ya wanakijiji wanamalizia sherehe za mwisho wa mwaka kwa kucheza ngoma za vijana wao wa kike (Wali) ambayo wamefikia umri kuanzia miwaka 14 hadi 17.

Wanakijiji wa Kingolwira kwa mwaka huu kwenye tarehe ya 08DEC, upepo mkali na usiku kiasi saa 3 na nusu ilitokea tetemeko dogo la ardhi ambalo halikuleta madhala (sio hatari) ni mara chache sana kutokea tetemeko.

Kama kawaida wanakijiji cha Kingolwira ni wakulima, kwa hiyo msimu huu wanaandaa mashamba na wachache ndiyo wameanza kupanda mbegu shambani. Pia huu ni wakati wa kuvuna baadhi ya matunda kama embe, nanasi na kiasi kidogo cha machungwa.

Kwa kuwa wakati huu ni mapumziko ya shule wanafunzi wanashirikiana na wazazi wao katika kazi za shamba nyakati za asubuhi na jioni. Wanafunzi hushiriki katika michezo-kama mpira, na kucheza ngoma.

(28/12/2007)


 年末の今ごろのキンゴルウィラ村の天気は、雨がほどほどに降り、昼間はかなり暑いです。次の農耕シーズンの準備をする時期ですが、ある人たちは14歳から17歳の年齢に達した娘たち(Wali)の踊りという年末のお祭りを終えようとしています。

 今年キンゴルウィラ村の村人たちは、風の強い12月8日夜半21時30分ころに小さな地震を経験しましたが、被害はありませんでした(危険はなかった)。地震があるのは珍しいです。

 普通のキンゴルウィラ村の村人たちは農民ですから、この時期はそれぞれの畑の準備をしており、少数ですが既に種を播いた人たちもいます。また今は果物の収穫期度もあり、マンゴー、パイナップル、また少しですがオレンジが獲れます。

 この時期は学校は休みなので、子どもたちは親の畑仕事の手伝いを朝夕にしています。子どもたちはサッカーや踊りに興じてはいません。

(2007年12月28日)

村の家の前
サイザル麻畑のそばの道

閲覧数:0回0件のコメント

最新記事

すべて表示

JATAツアーズのスタッフたちが綴るタンザニアをご紹介します。 ​【目次】 ​ ★Kusikia si kuona(百聞は一見にしかず) - 相澤 俊昭 ★Tunatembea - 白川 千尋 ​ ★Habari kutoka Lukani(ルカニ村ニュース) - アレックス(ルカニ村出身) ​ ★Habari kutoka Kingolwira(キンゴルウィラ村ニュース) - グビ、ハミシ、ヤウ

記事: Blog2_Post
bottom of page